Pata taarifa kuu
CHAD-MALI-UFARANSA-Ugaidi-Usalama

Kusini mwa jangwa la Sahara: Operesheni Barkhane Yaanza

Kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa walioko kusini mwa jangwa la Sahara wameanza ijumaa wiki hii opereshi iitwayo Barkhane, baada kukamilika kwa operesheni Serval nchini Mali.

Ndege zisiyo na rubani zitatumiwa katika operesheni Barkhane kusini mwa jangwa la sahara.
Ndege zisiyo na rubani zitatumiwa katika operesheni Barkhane kusini mwa jangwa la sahara. RFI/ Pierre Firtion
Matangazo ya kibiashara

Kikosi hicho kitaendesha harakati zake kuanzia nchini Chad hususan katika mji wa Ndjamena, wanajeshi wa Ufaransa waliokua katika maeneo ya jangwa la Sahara yalitumwa hivi karibuni kusini mwa jangwa la sahara kuungana na wenzao katika operesheni Barkhane.

Tofauti na operesheni Serval, operesheni hii mpya ya kikosi cha Ufaransa Barkhane itaendeshwa katika mataifa mbalimbali yalioko kusini mwa jangwa la Sahara, jambo ambalo linaweza likasababisha kutokea kwa matatizo kuhusu uhuru wa wa mataifa.

Operesheni hiyo Barkhane itaendeshwa na kikosi cha wanajeshi 3000, 1000 katika jimbo la Gao na 1200 nchini Chad,na lengo la operesheni hiyo ni kukabiliana na ugaidi ambao umekua sugu katika mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara.

Vifaru na magari magari mengine ya kivita hayatatumiwa katika operesheni hiyo ya Barkhane. Lakini ndege za kivita na zile zisiyo na rubani zitatumiwa katika operesheni.

Wakati huo, viongozi wa Ufaransa watashirikiana na viongozi wa mataifa hayo kunakoendeshwa operesheni Barkhane. Awali serikali ya Mali ililituhumu jeshi la Ufaransa kutoipa taarifa yoyote kuhusu operesheni zake.

Operesheni hiyo itaongozwa na jenerali Palasset aliyeongoza operesheni Serval nchini Mali, makao makuu ya kikosi hicho yamewekwa katika mji wa Ndjamena.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.