Pata taarifa kuu
UN-SIKU YA MANDELA-

UN : siku ya Mandela yasheherekewa duniani

Hii leo ni siku ya ijumaa tarehe 18 mwezi julai, ambapo Dunia Inasherehekea "Siku ya Mandela" kwa mara ya kwanza baada ya kifo cha rais huyo wa kwanza mweusi nchini Afrika Kusini.

Aliye kua rais wa Afrika Kusini akiwa mia mwasisi wa harakati za ubauzi wa rangi, Mzee Nelson Mandela "Madiba" 1918-2013
Aliye kua rais wa Afrika Kusini akiwa mia mwasisi wa harakati za ubauzi wa rangi, Mzee Nelson Mandela "Madiba" 1918-2013 Reuters
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa ulitangaza siku hii kuwa siku mahsusi kwa Nelson Mandela, muasisi wa harakati za kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Nelson Mandela ambaye alifariki Desemba 5 mwaka 2013, angelitimiza miaka 96 ijumaa wiki hii. Kila mmoja ametakiwa kwa tarehe ya leo Julai 18 kuwajibika kwa muda wa dakika 67 kwa kutendea mazuri wenzao, ili kuenzi harakati za Nelson Mandela Madiba za kupambana na ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini ziliyopelekea taifa hilo kuondokana na siasa hizo, Umoja wa Mataifa umebainisha.

Mazishi ya Nelson Mandela Madiba.
Mazishi ya Nelson Mandela Madiba. REUTERS/SABC via Reuters

Mwaka wa 2009, baada ya kuteuliwa siku hii, miji miwili Jahannesburs na New York ilianzisha rasmi siku mahsusi kwa Mandela. Mawaka 2014 matifa 126 duniani yamesheherekea siku hii, huku kukiwa kumeandaliwa maandamano zaidi ya 1000”, mkurugenzi wa taasisi ya kuwahudumiya watu wasiyojiweza iliyoanziushwa na Mandela, Sello Hatang, amesema akijisifu.

Nchini Afrika Kusini, rais Jacob Zuma amewatolea wito wananchi wa taifa hilo kufanya usafi barabarani na sehemu zote ili kuunga mkono harakati za mtangulizi wake Nelson Mandela Madiba.

“Tunapaswa kuonesha uzalendo wetu kwa taifa letu zuri, hasa kufanya usafi kwa ushirikiano. Kwa mantiki hii tutashirikiana kwa kulijenga taifa letu zuri, kama alivyotufunza Madiba”, amesema Jacob Zuma.

Shughuli hiyo imefanyika katika kijiji cha Mvezo, alikozaliwa Nelson Madiba Mandela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.