Pata taarifa kuu
KENYA-Sheria

Kenya : ofisi ya mashitaka yaomba kuongezewa muda

Gavana wa kaunti ya Lamu, Issa Timamy anaendelea kufuatiliwa na ofisi ya mashitaka nchini Kenya kwa tuhuma za kuhusika na mauaji, ugaidi na kuwasafirisha watu ili kujiunga na makundi ya kigaidi.

Wahanga katika mashambulizi yaliyotokea Mpeketoni, karibu na kaunti ya Lamu wasafirishwa hospitalini.
Wahanga katika mashambulizi yaliyotokea Mpeketoni, karibu na kaunti ya Lamu wasafirishwa hospitalini. AFP/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Hapo jumanne wiki hii, upande wa mashitaka umeomba mahakama ya Kenya iongeze miezi miwili ili iwe imekamilisha faili dhidi ya gavana wa kaunti ya Lamu, kusini mashariki mwa Kenya akishukiwa kuhusika katika mauaji yaliyotokea hivi karibuni katika kaunti hio.

Issa Timamy, alikamatwa Juni 25 kwa uchunguzi wa mauaji na ugaidi. Lakini aliachiwa huru kwa dhamana Juni 30 na vyombo vya sheria vya Kenya, baada ya kufutilia mbali madai ya ofisi ya mashitaka ya kutaka azuiliwe kwa siku 14, muda ambao uchunguzi utakua umekamilika.

wanawake wa kijiji cha Pandanguo,  Juali 11 mwaka 2014, baada ya shambulio la usiku.
wanawake wa kijiji cha Pandanguo, Juali 11 mwaka 2014, baada ya shambulio la usiku. REUTERS/Siegfried Modola

Mwakilishi wa ofisi ya mashitaka, Alexander Muteti, ambae angepaswa kuonyesha mahakama ushahidi tosha wa mashitaka dhidi ya Issa Timamy, ameomba aongezewe muda ili aweze kuwatafuta mashahidi waliokimbia eneo la tukio kwa kuhofia usalama wao.

“Raia wengi walihama makaazi yao na ni vigumu kuwapata, na hali hio ndiyo husababisha uchunguzi wetu unakwama. Kwa hiyo tumekua tunaomba mahakama ituongeye muda ili tuweze kukamilisha na kurejea mbele ya mahakama hii”, amesema Muteti.

Wanasheria wa Timamy, wamebaini kwamba madai hayo hana msingi, wakisema kwamba upande wa mashitaka hawana ushahidi dhidi ya mteja wao.

Takriban watu 87 waliuawa tangu katikati ya mwezi wa Juni katika mashambulizi mfululizo yaliyokua yakitokea usiku katika vijiji viliyo karibu na kaunti ya Lamu. Mashambulizi hayo yalidaiwa kutekeleza na wanamgambo wa kundi la Al Shabab lenye mafungamano na kundi la Al Qaeda, wakidai kwamba ni ulipizaji kisase dhidi ya wanajeshi wa Kenya nchini Somalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.