Sudani Kusini yaadhimisha miaka mitatu ya uhuru
Nchi ya Sudan kusini ambayo ni taifa changa duniani inasherehekea hii leo miaka mitatu ya uhuru wake katika muktadha wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, baada ya miezi kadhaa ya mauaji ya kikabila. Tifa hilo pia linakabiliwa na kitisho cha njaa.
Imechapishwa:
Vita hivyo ambavyo vinavyotokana na malumbano kati ya rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar vimesababisha watu wasiopungua milioni moja na nusu kuyakimbia makazi yao na mamia kwa maelfu kuuwawa.
Raia wa Sudan Kusini "ni waathirika wa kwanza wa vita hivyo ambavyo kwa mujibu wa wadadisi vinaiathiri nchi hiyo katika nyanja zote.
Sudani Kusini ilipata uhuru wake Julai 9 mwaka 2011, baada ya kujitenga na khartoum.
Hata hivo taifa la Sudani Kusini linakabiliwa na baa la njaa. Hayo yanathibitishwa na shirika la kihisani la Oxfam.
“Sudani Kusini inakabiliwa wakati huu na tatizo kubwa, ambapo watu takriban milioni 4 sawa na theluthi moja ya raia wake wanakabiliwa na baa la nja, huku msaada unaotolewa kwa walengwa ukiwa hautoshi, limesema shirika hilo la Oxfam, likibaini kwamba nusu ya watu hao ndio wananufaika na msaada huo.
Katika maeneo kadhaa hususan Jonglei (mashariki), jamii za wafugaji wamepoteza mifugo yao, huku wakulima wakiwa hawana mbegu wakati zinasalia siku chache ili msimu wa kulima ufikiye ukingoni.
Njaa hio imesababisha takriban watu 100.000 wanayahama makaazi yao na kuomba hifadhi kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa.