Pata taarifa kuu
KENYA-CORD-Maandamano-Siasa-Usalama

Kenya : upinzani waandamana kwa shida

Mamia kwa maelfu ya wakenya wameandamana jumatatu ya wiki katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, dhidi ya rais Uhuru Kenyatta. Maandamanao yamefanyika wakati ambapo taharuki imetanda nchioni humo baada ya mashambulizi ya hivi karibuni yaliyosababisha maafa karibu na eneo la kitali.

Waandamanaji kwenye eneo la Uhuru Parc mjini Nairobi nchini Kenya.
Waandamanaji kwenye eneo la Uhuru Parc mjini Nairobi nchini Kenya. REUTERS/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa CORD wakiongozwa na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga, aliyekuwa makamu wa rais Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula waliandaa mkutano wa kisiasa jana jijini Nairobi na kuzindua vuguvugu linalofaghamika kama Okoa Kenya.

Miongoni mwa maazimio hayo ni pamoja na kutaka tume ya uchaguzi nchini humo kufutwa, majeshi ya Kenya nchini Somalia kurudi nyumbani na kukomeshwa kwa ufisadi.

“Uhuru anapaswa kuondoka”, umekua ukilalamika umati wa waandamanaji ambao wamekua wamekusanyika katika eneo moja la mji wa Nairobi, askari polisi na wanajeshi wakipelekwa kwa wingi katika eneo hilo.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga.
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga. REUTERS/Thomas Mukoya

“Wakenya wanataka suluhu lipatikane katika sekta ambazo zinakabiliwa na vurugu”, amesema kiongozi wa upinzaini akiwa pia muanzilishi wa maandamano hayo, Raila Odinga, akikemeya vikali hali ya usalama ambayo inaendelea kudorora pamoja na maisha kuwa duni.

Kabla ya hotuba ya kiongozi huyo wa upinzani, asakri polisi na wanajeshi walifyatua mabomu ya kutoa machozi ili kutawanya waandamanaji ambao walikua wakiwarushia mawe. Katika kaunti ya Kisumu, magharibi mwa nchi, ambayo ni ngome ya kiongozi wa upinzani, mamia ya vijana waliokua na hasira waliandamana, lakini walitawanywa na mabomu ya kutoa machozi yaliyofyatuliwa na polisi.

Eneo la Uhuru, kulikofanyika maandamano lina tafsiri kubwa, kulingana na mafaanikio makubwa yaliyopatikana kupitia maandamano ya mwaka 1990 ya kudai mfumo wa vyama vingi yaliyoandaliwa na upinzani kipindi hicho.

Upinzani unautuhumu utawala kuweka mbele siasa za kibaguzi.

Miongoni mwa maazimio hayo ni pamoja na kutaka tume ya uchaguzi nchini humo kuvunjiliwa mbali, majeshi ya Kenya yaliyoko nchini Somalia kurudi nyumbani na kukomeshwa kwa ufisiadi.

Polisi iliwapeleka askari polisi 15000, wakati nchi ya Kenya inakabiliwa na mdororo wa kiusalama kutokana na mashambulizi ya wanamgambo wa kundi la Al Shabab lenye mafungamano na kundi la Al Qaeda. Mashambulizi hayo ni kama fimbo ya adhabu kwa taifa hilo la Afrika Mashariki kutokana na kuwatuma wanajeshi wake nchini Somalia.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta. Kenyagvt

Serikali ya rais Uhuru Kenyatata, imekataa kuzungumza na upinzani na badala yake kutaka upinzani kufikisha shuinikizo zao bungeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.