Pata taarifa kuu
DRC-MONUSCO-HRW-Haki za binadamu

HRW yanyooshea kidole cha lawama jeshi la Congo na kikosi cha Monusco

Shirika la kimataifa linalo tetea haki za binadamu lenye makao yake makuu nchini Marekani la Human Right Watch limelituhumu jeshi la jamhuri ya kidemokrasia ya Congo la FARDC pamoja na vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini humo Monusco kwa kupuuzia kuzuia kutokea kwa machafuko ya mwezi uliopita huko mashariki mwa DRCongo.

Wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Congo (Monusco) wakipambana dhidi ya makundi ya waasi..
Wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Congo (Monusco) wakipambana dhidi ya makundi ya waasi.. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo limesema majeshi ya Congo na yale ya Monusco hayakuingilia kati ili kukomesha machafuko yaliogharimu maisha ya watu zaidi ya 30 na ambayo yalitokea katika kijiji cha Mutarule katika usiku wa Juni 6 kuamkia Juni 7 katika mkoa wa Kivu ya Kusini

Mkuu wa ofisi ya MONUSCO wilayani Uvira, Ould Mohamed El Hacen (amevaa shati nyeupe) akiwa na jenerali Carlos Alberto dos Santos Cruz, mbele ya moja ya nymba ziliyochomwa moto katika machafuko ya kikabila yaliyotokea Mutarule, mkoani Kivu Kusini..
Mkuu wa ofisi ya MONUSCO wilayani Uvira, Ould Mohamed El Hacen (amevaa shati nyeupe) akiwa na jenerali Carlos Alberto dos Santos Cruz, mbele ya moja ya nymba ziliyochomwa moto katika machafuko ya kikabila yaliyotokea Mutarule, mkoani Kivu Kusini.. MONUSCO / Laurent Sam Oussou

Shirika hilo limeendelea kuwa wanajeshi hao waliwaacha wananchi wa Mutarule waendelee kuuawa wakati ambapo kulikuwa na taarifa za kutokea kwa machafuko hayo na ambapo wananchi waliomba msaada tangu tu yalipoanza machafuko hayo na walikuwa karibu wangeliweza kuingilia kati.

Hivi karibuni kiongozi wa majeshi ya Monusco nchini DRCongo Martin Koble alibaini maskitiko yake kuona vikosi vya Umoja wa Mataifa vilishindwa kuziia mauaji hayo yasitokei.

Wanajeshi wa kikosi cha Monusco wakishirikiana na wanajeshi wa Congo FARDC kwa kuyasaka makundi ya waasi mashariki mwa Congo.
Wanajeshi wa kikosi cha Monusco wakishirikiana na wanajeshi wa Congo FARDC kwa kuyasaka makundi ya waasi mashariki mwa Congo. RFI/LL.Westerhoff

Shirika hilo limesema hakuna muhusika hata mmoja wa mauaji hayo aliyekamatwa, hivyo Human rights watch limeilitolea wito jeshi la FARDC na Umoja wa Mataifa nchini DRCongo Munusco kuchunguza nini kilichotokea na kuhakikishi mauaji kama hayo hayatokei tena.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.