Pata taarifa kuu
NIGERIA-Usalama

watu zaidi ya 50 wauawa kaskazini mashariki mwa Nigeria

Shambulio la mwisho linalodaiwa kutekelezwa na kundi la wanamgambo wa kislam la Boko Haramu, katika kanisa zilioko kaskazini mashariki mwa Nigeria, limesababisha vifo vya watu 54, amesema mmoja wa viongozi tawala wa jimbo la Borno, ambae hakutaka jina lake litajwe. Mashambulizi hayo yalitokea katika vijiji vinne viliyo karibu na mji wa Chibok, walikotekwa nyara wasichana zaidi ya 200 katikati ya mwezi Aprili.

Rais wa Nigeria Goodluk Jonathan akiozungumza kusu hali ya usalama inayojiri kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Rais wa Nigeria Goodluk Jonathan akiozungumza kusu hali ya usalama inayojiri kaskazini mashariki mwa Nigeria. REUTERS/Afolabi Sotunde/Files
Matangazo ya kibiashara

Mashahidi wanasema kwamba wanamgambo hao, ambao walikua kwenye pikipiki, walirusha mabomu katika kanisa za Kwada, Ngorujina, Karagau pamoja na Kautikari wakati wa umini wa kikristo walikua katika ibada ya jana jumapili.

Kwa mujibu wa kiongozi wa tawala wa mji wa Chibok, ambae pia hakutaka jina lake litajwe, wakaazi wa mji huo wamegundua miili 47 katika msitu, lakini zoezi la kutafuta miili mingine bado inaendelea, huku akibaini kwamba huenda idadi ya waliouawa ikaongezeka.

Msemaji wa serikali ya Nigeria, Mike Omeri, ameiambia AFP kwamba idadi kadhaa ya watu waliuawa, huku akibaini kwamba hajapata idadi rasmi kutoka kwa viongozi tawala katika vijiji hivyo.

Akihojiwa kuhusu taarifa zinazosema kwamba jeshi lilifahamishwa na raia kuwa maisha yao yako hatarini bila hata hivo kuwasili kwenye maeneo ya tukio, Omeri amesema” Nilipata (...) taarifa za uhakika kwamba jeshi la aridhini liliwasili kwenye maeneo ya tukio. Huenda lilichelewa kuwasili, lakini liliwasili kwenye maeneo hayo”.

Kwa mujibu wa kiongozi wa Chibok, jeshi halikujaribu hata mara moja kuwasili kwenye maeneo ya tukio.

“wanaosema kuwa jeshi liliwasili kwenye maeneo ya tukio si kweli”, kiongozi huyo ameambia AFP.

Wanajeshi wa Nigeria katika mji wa Baga, katika jimbo la Borno.
Wanajeshi wa Nigeria katika mji wa Baga, katika jimbo la Borno. AFP PHOTO / PIUS UTOMI EKPEI

Jimbo la Borno limekua likishambuliwa na wanamgambo wa kislam wa kundi la Boko Haram. Mashambulizi ya kundi hilo yamesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha katika kipindi cha miaka 5, na karibu watu 2.500 tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.