Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Mwanamke aliyekataa kuasi Ukristo nchini Sudan bado anahojiwa na polisi

media Meriam Yahia Ibrahim Ishag, akiwa na mwanaye

Wakili wa Mwanamke Mkristo raia wa Sudan Meriam Yahia Ibrahim Ishag, anasema mteja wake  yuko salama na  anaendelea kuhojiwa na maafisa wa polisi jijini Khartoum kutokana na tuhma za kughusi kibali cha kuondoka nchini humo.

 

Merium mwenye umri wa miaka 26 akiwa na mume wake alizuiliwa kuondoka nchini humo siku ya Jumanne, siku moja tu baada ya hukumu yake ya kunyongwa kwa kosa la kuasi Uislamu kufutwa na Mahakama ya rufaa.

Wakili wake, Mohanad Mustafa amesema mwanamke huyo hajakamatwa kama ilivyokuwa imeripotiwa hapo awali na vyombo vya habari ila tu anahojiwa ni kwanini anataka kuondoka nchini humo haraka baada ya hukumu yake kufutwa.

Mumewe raia wa Marekani Daniel Wani na watoto wao wawili wote wako pamoja naye wakati mahojiano hayo yanapoendelea, lakini anasema wanatamani kuondoka nchini Sudan haraka iwezekavyo kwa kile wanachosema ni kuhofia usalama wao.

Aidha, wakili huyo amekataa kusema ni nchi gani mteja wake anakimbilia.

Polisi jijini Khartoum wanasema Merium hakuwa na vibali halali za kuondoka nchini humo na pia ni sababu ya yeye kuhojiwa.

Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani nayo imesema Meriam hajakamatwa, na serikali ya Khartoum imeihakikishia kuwa yuko salama na ataachiliwa huru.

Hukumu dhidi ya Ishag mwezi uliopita ililaaniwa na Jumuiya ya Kimataifa na Mashirika ya kutetea haki za Binadamu yaliyosema hatua ya Mahakama ya Khartoum ilikwenda kinyume na haki za kuabudu.

Mbali na Mashirika hayo ya kutetea haki za Binadamu yakiwemo Human Righst Watch na Amnesty International, zaidi ya watu Milioni moja walitumia tovuti ya Change.org kuendelea na shinikizo za kutaka kuachiliwa kwa mwanamke huyo.

Meriam akiwa na mme wake Dani Reuters

Babake Merium alikuwa Mwislamu na mamake Mkiristo wa dhehebu la Orthodox kutoka nchini Ethiopia na hatua yake ya kutaka kuolewa na Mkiristo ilimletea matatizo na kukataa kuikana dini yake.

Mahakama ilikuwa imemhukumu kunyongwa kutokana na sheria ya Kiislamu ya mwaka 1983 kuwa mtu hastahili kuikana dini ya Kiislamu na hukumu yake ni kifo.

Meriam  alipokuwa na umri wa miaka mitano, babake yake ambaye alikuwa Mwislamu aliiacha familia yake na akalelewa kwa misingi ya dini ya Kikiristo upande wa mamake.

Mwanamke huyo ambaye alijiifungulia jela, alikuwa anatoroka Sudan kwa kuhofia usalama wake baada ya kuachiliwa huru.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana