Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Waislamu 17 wauliwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Watu waliojihami kwa silaha wamewaua Waislamu 17 katika kambi ya wakimbizi  jijini Bangui nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Wapiganaji wa Seleka
Wapiganaji wa Seleka REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Haya ndio mauaji ya hivi karibuni ya kidini nchini humo kwa mujibu wa ripoti za wanajeshi wa Kimataifa wa kulinda amani nchini humo.

Wapiganaji wa Anti- Balaka wanaoegemea mrengo wa Wakikiristo ndio waliotekeleza mauaji hayo siku ya siku ya Jumatatu kwa mujibu wa ripoti hizo.

Wakati mauaji hayo yakitokea, Mashirika ya kutetea haki za Binadamu nchini humo FIDH yanasema visa vya ukiuwkaji wa haki za binadamu vinatekelezwa nchini humo.

Ripoti ya mashirika hayo iliyopewa jina “ Ni sharti waondoke wote au wafe”, inaeleeza kuwa kinachotokea nchini humo ni mapambano ya kutaka madaraka ambayo yamechukua mrengo wa kidini kati ya Wakiristo na Waislamu nchini humo.

Raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wakizuia barabaara jijini Bangui
Raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wakizuia barabaara jijini Bangui AFP PHOTO / MARCO LONGARI

Tangu mwezi Desemba mwaka 2013 jijini Bangui, wapiganaji wa Anti- Balaka wamekuwa wakitekeleza mauaji dhidi ya Waislamu nchini humo kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Kundi la Wailsmau la Seleka pia bado linaendelea kutekeleza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Ripoti hiyo inamtaja  rais wa zamani Michel Djotodia, aliyekuwa Mkuu wa kitengo chake cha Inteljensia Noureddine Adam na kiongozi wa kundi la wapigaji wa Janjaweed nchini Sudan Jenerali Moussa Assimeh kuhusika moja kwa moja na mauaji nchini humo.

Raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wakikimbizwa hospitalini
Raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wakikimbizwa hospitalini AFP PHOTO/MARCO LONGARI

Zaidi ya watu 3,000 wamepoteza maisha nchini humo, Maelfu wamejeruhiwa na mamia ya wanawake kubakwa wakati wa  vita hivi.

Mashirika hayo ya haki za binadamu yanataka Jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati kinachoendelea na Mahakama ya Kimataifa ya ICC kuendelea na uchunguzi wake ili kuwafungulia haraka mashitaka wanaohusika na visa hivyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.