Pata taarifa kuu
KENYA

Kundi la Al Shabaab lajigamba kuhusika katika mauaji ya Watu 48 kwenye pwani ya Kenya

Polisi nchini Kenya wanasema watu 48 wameuliwa na wengine kujeruhiwa katika mji wa Mpeketoni katika Kaunti ya Lamu Pwani ya Kenya baada ya watu waliojihami kwa silaha kuvamia mji huo Jumapili usiku. Polisi wanasema huenda idadi ya vifo ikaongezeka, baada ya kundi hilo linaloaminiwa kuwa la Al Shabab kutoka nchini Somalia kutekeleza shambulizi hilo baya katika siku za hivi karibuni nchini humo. 

Gari lililoteketezwa moto mjini  Mpeketoni
Gari lililoteketezwa moto mjini Mpeketoni Standard Newspaper Kenya
Matangazo ya kibiashara

Walioshuhudia mashambulizi hayo wanasema, watu hao walifwatulia risasi watu katika makaazi yao, wakateketeza moto majengo mbalimbali, maeneo ya biashara na Benki.

Inspekta wa Polisi David Kimaiyo amesema idadi ya wapiganaji hao ilikuwa ni zaidi ya 50 ambao walikuwa wamejihami kwa silaha hatari zikiwemo vilipuzi walizotumia kutekeleza mashambulizi hayo.

Kimaiyo ameongeza kuwa kwa sasa juhudi zinaendelea kutafuta miili zaidi na waliotekeleza mashambulizi hayo hawajulikani walipo.

Hadi sasa hakuna kundi lolote lililojitokeza kudai kutekeleza uvamizi huo hilo lakini vyombo vya ulinzi nchini humo vinasema vinaaminini ni kundi la Al Shabab ambalo limekuwa likitekeleza mashambulizi hayo nchini humo.

Msemaji wa Jeshi la Kenya Meja Emmanuel Chirchir kupitia ukurasa wake wa Twitter alinukuliwa akisema “ Watu hao waliwalemea polisi na kuanza kuwafwatulia watu risasi”.

Ndege za polisi zimepaa zimeendelea kudadisi maeneo ya Mpeketoni hadi Lamu  huku polisi wakikabiliana vikali wakiwa ardhini.

Ukosefu wa usalama hasa Pwani ya Kenya imesabisha kuondoka kwa watalii katika eneo hilo na nchi ya Uingereza Ijumaa iliyopita ilifunga Ubalozi wake mdogo mjini Mombasa kwa hofu ya usalama.

Kundi la kigaidi la Al Shabab limeendelea kuionya serikali ya Kenya kuwa ikiwa haitawaondoa wanajeshi wake nchini Somalia mashambulizi hayo yataendelea.

Mwaka uliopita, shambulizi lingine baya lilitekelezwa na kundi hilo jijini Nairobi katika jengo la Kibiashara la Westgate na kusabibisha vifo vya watu 67.

Kenya ilituma wanajeshi wake nchini Somali mwaka 2011 kupambana na kundi la kigaidi la Al Shabab.

Viongozi wa serikali ya Kenya wamejiapiza kukabiliana na mashambulizi hayo huku wakisema kuwa hayawezi kuwapelekea wao kuondoa sehemu kubwa ya wanajeshi wao katika nchi ya Somalia.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.