Pata taarifa kuu
NIGERIA

Mamia ya watu wahofiwa kuuawa kwenye shambulio la Boko Haram kaskazini mwa Nigeria

Mamia ya raia wa Nigeria kaskazini mwa nchi hiyo wanahofiwa kuuawa kwenye miji mitatu tofauti kufuatia mashambulizi yaliyotekelezwa usiku wa kuamkia leo na wapiganaji wanaodhaniwa kuwa ni kutoka kundi la Boko Haram. 

Baadhi ya raia wa jimbo la Borno kaskazini mwa Nigeria wakiwa na silaha za jadi kwaajili ya kujihami na wapiganaji wa Boko Haram
Baadhi ya raia wa jimbo la Borno kaskazini mwa Nigeria wakiwa na silaha za jadi kwaajili ya kujihami na wapiganaji wa Boko Haram REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa jadi katika kitongoji cha Gwoza kwenye jimbo la Borno wamesema kuwa inakadiriwa kuwa watu kati ya 400 na 500 waliuawa kwenye shambulio la kushtukiza lililotekelezwa a wapiganaji hao wa Boko Haram.

Iwapo Serikali ya jimbo la Borno itatangaza idadi rasmi ya watu waliouawa kwenye shambulio hili kwenye miji ya Goshe, Attagara, Agapalwa na Aganjara basi hii itakuwa ni idadi kubwa zaidi ya watu kuuawa kwenye shambulio la kundi hili katika kipindi cha miaka mitano.

Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi za Serikali ya Nigeria kuthibitisha idadi kamili ya watu waliouawa kwenye shambulio hili, ingawa mashirika ya kutetea haki za binadamu yanadai kuwa idadi huenda ikawa kubwa zaidi.

Wapiganaji wa Boko haram wanadaiwa kutumia silaha kubwa kubw akutekeleza mauaji hayo ambapo pamoja na kuwafyatulia wananchi risasi, walichoma moto nyumba za wakazi wa miji hiyo.

Mmoja wa wabunge kwenye bunge la kitaifa, Peter Biye anasema "Mauaji ni makubwa sana lakini hakuna yeyote anayeweza kutoa idadi kamili ya waliouawa kwakuwa hakuna aliyeweza kufika kwenye eneo la tukio kwasababu bado wapiganaji hao wako huko". Alisema Biye.

Waandamanaji wa Nigeria wakiwa na mabango ya kutaka kuachiwa kwa wasichana wa shule wanaoshikiliwa na Boko Haram
Waandamanaji wa Nigeria wakiwa na mabango ya kutaka kuachiwa kwa wasichana wa shule wanaoshikiliwa na Boko Haram REUTERS/Akintunde Akinleye

Mamia ya wananchi wameripotiwa kuyakimbia makazi yao kuhofia kuuawa na wapiganaji hao ambao safari hii walienekana kuwa wamejipanga katika kutekeleza kile ambacho wamekifanya kwenye jimbo la Borno.

Hapo jana watu 45 waliripotiwa kuuawa kwenye kijiji cha Barderi jirani na jimbo la Borno ambapo wapiganaji wa Boko Haram waliojifanya ni wahubiri wa kidini na kisha wakaanza kuwafyatulia risasi wananchi waliohudhuria.

Mashambulizi haya yanatekelezwa wakati huu ambapo jeshi la Nigiria likisaidiwa na wanajeshi wa Marekani na mataifa mengine ya Ulaya wakiendesha operesheni ya kuwasaka wapiganaji hao kwenye maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.