Pata taarifa kuu
SUDAN

Serikali ya Sudan kumwachia huru mwanamke aliyehukumiwa kunyongwa

Siku moja baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa huenda utawala wa Khartoum nchini Sudan ukamwachia huru msichana aliyehukumiwa adhabu ya kifo kwa madai ya kukana dini yake, mme wamsichana huyo amedai kutokuwa na taarifa zozote kuhusu uamuzi huo. 

Meriam akiwa na mme wake Dani
Meriam akiwa na mme wake Dani Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Sudan, imesema kuwa siku yoyote kuanzia sasa, Meriam yahia Ibrahim Ishag ataachiwa huru.

Hukumu hiyo ambayo ilivuta hisia kali toka Jumuiya ya Kimataifa ambayo ililaani hukumu hiyo kwa kile mataifa ya magharibi na wanaharakati wanadai ililenga kuminya uhuru wa mtu kuabudu dini anayotaka.

Wanawake wa Sudan wakiandamana mjini Khartoum kupinga kuhukumiwa kwa mwenzao
Wanawake wa Sudan wakiandamana mjini Khartoum kupinga kuhukumiwa kwa mwenzao REUTERS

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Sudan, Abdullah al-Azraq amethibitisha mpango wa Serikali kutaka kumuachia huru msichana huyo ambayo juma lililopita alijifungua akiwa gerezani.

Hata hivyo wizara hiyo haikuweka wazi sababu za kufikiria upya hukumu hiyo na hatua ya kumuachia huru, Meriam, ila wachambuzi wa mambo wanaona kuwa ni kutokana na shinikizo kubwa toka Jumuiya ya Kimataifa.

Mme wa msichana huyo ambaye ni raia wa Marekani, Daniel Wani amesema hajapokea taarifa zozote kuhusu hatua ya Serikali kutaka kumuachia huru mke wake na kuongeza kuwa alikataliwa kumuona mke wake juma lililopita.

Ishag ambaye alizaliwa na baba wa Kiislamu aliiambia mahakama kuwa hakuwahi hata siku moja toka amezaliwa kusali kwenye dini ya baba yake na badala yake mara zote amekuwa akienda kanisani akifuata dini ya mama yake.

Mahakama ilimpa siku tatu ya kufikiria uamuzi wake lakini alikataa kubadili uamuzi wake na mahakama kuamua kutoa hukumu ya kifo dhidi yake.

Kwa mujibu wa Sharia ya Sudan, inakataza msichana yeyote kuoelewa na mtu wa dini tofauti na ile ya wazazi wake ambapo Ishag alihukumiwa adhabu ya viboko 100 na adhabu ya kifo.

Mwishoni mwa juma waziri mkuu wa Uingereza David Cameron alieleza kusikitishwa na hukumu hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.