Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM

Kundi la Boko Haram lazidisha mashambulizi licha ya Serikali ya Nigeria kutangaza vita dhidi yake

Hali ya wasiwasi imeendelea kutawala kaskazini mwa nchi ya Nigeria kufuatia mashambulizi mfululizo kwenye vijiji vinnne tofauti, mashambulizi yanayodaiwa kutekelezwa na wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram. 

Wananchi wa Nigeria wakipita kwenye moja ya eneo lililoshambuliwa na Boko Haram
Wananchi wa Nigeria wakipita kwenye moja ya eneo lililoshambuliwa na Boko Haram REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mashuhuda wa mashambulizi hayo wamedai kuwa kundi la watu wenye silaha walivamiwa kwenye vijiji vyao na kuanza kufyatua risasi hovyo pamoja na kulipua mabomu.

Askari wa Nigeria wakifanya uchunguzi kwenye moja ya eneo lililoshambuliwa na Boko Haram
Askari wa Nigeria wakifanya uchunguzi kwenye moja ya eneo lililoshambuliwa na Boko Haram REUTERS/Afolabi Sotunde

Jeshi la Nigeria mpaka sasa halijasema chochote kuhusu tukio hili lililotekelezwa kaskazini mwa nchi hiyo, eneo ambalo wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakitekeleza mauaji dhidi ya raia.

Vijiji vilivyokuwa vimelengwa na wapiganaji hao ni pamoja na Gamboru Ngala kijiji kilichopo kwenye mpaka na nchi ya Cameroon eneo ambao kwa mwezi uliomazika wametekeleza mashambulizi mengi zaidi.

Mashambulizi ya mwishoni mwa juma yalilenga vijiji vya Nuwari, Musari na Walori ambapo watu wenye silaha wakiwa wamevalia sare za jeshi wakiwa kwenye magari walianza kufyatua risasi.

Watu kumi na tano wameripotiwa kuuawa kwenye mashambulizi haya ingawa mashirika ya kutetea haki za binadamu kaskazini mwa nchi hiyo yanadai kuwa huenda idadi hiyo ikawa kubwa zaidi.

Wasichana wanafunzi ambao wanashikiliwa na kundi la Boko Haram
Wasichana wanafunzi ambao wanashikiliwa na kundi la Boko Haram

Mashambulizi haya yanatekelezwa wakati huu, jeshi la Serikali kwa kushirikiana na vikosi maalumu vya kigeni vilivyoko nchini humo katika harakati za kuwasaka wapianaji hao ambao wamewateka wasichana washule zaidi ya 200.

Serikali ya Nigeria imejikuta iko kwenye shinikizo kubwa toka kwa wanaharakati na familia za wasichana hao ambao wanataka kuongezwa kwa nguvu zaidi ya kuwasaka wasichana hao ambao bado wanashikiliwa na kundi hilo.

Juma moja lililopita viongozi wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika ECOWAS walikutana nchini Ghana kujadili hali ya usalama nchini Nigeria na Mali ambapo walikubaliana kushirikiana katika harakati za kuyakabili makundi ya kigaidi kwenye nchi zao.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande akiwa na viongozi wa mataifa ya Afrika Magharibi
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande akiwa na viongozi wa mataifa ya Afrika Magharibi

Rais Goodluck Jonathan ametangaza vita dhidi ya kundi hilo na kukataa kuwa na mazungumzo na kundi hilo kuwezesha kuachiliwa kwa wasichana hao licha kuwa sasa rais wa zamani wa nchi hiyo, Olusegun Obasanjo kuanza mazungumzo na viongozi wa kundi hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.