Pata taarifa kuu
RWAND-HRW-Usalama-Haki za Binadamu

Rwanda: polisi yatupilia mbali tuhuma dhidi yake

Polisi nchini Rwanda imekanusha ripoti ya Shirika la Kimataifa la kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch inayoituhumu serikali ya Rwanda kutekeleza vitendo vinavyosababisha watu kutoweka na kupotelea kusikojulikana.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ambaye srikali yake inatuhumiwa kuwamalizia maisha baadhi ya wakimbizi wakinyarwanda waliyokimbilia nje ya nchi.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ambaye srikali yake inatuhumiwa kuwamalizia maisha baadhi ya wakimbizi wakinyarwanda waliyokimbilia nje ya nchi. AFP PHOTO / STEPHANIE AGLIETTI
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, msemaji wa polisi nchini humo ametupilia mbali taarifa hizi na kuzizungumzia kuwa ni habari za uongo na zisizo na msingi wala uhakika wowote, na kusema kuwa watu zaidi ya 35 tu ndio wamekamatwa kutokana na njama zao dhidi ya serikali na shughuli za kigaidi.

Wakati hayo yakijiri, mpinzani wa utawala wa Paul Kagame akiwa ukimbizini nchini Ubelgiji Faustin Twagiramungu ameweweka bayana vitisho vya kifo dhidi yake vinavyomkabili kama alivyotahadharishwa na vyombo vya Usalama nchini Rwanda.

“Nimepigiwa simu na kuambiwa kuwa twagiramungu uko hatarini kwa hiyo tunakutumia ulinzi na baada ya muda mfupi nikaona askari polisi wamewasili kwangu. Mkuu wa usalama wa taifa ameniambia kuwa ipo haja ya kunilinda na ndio maana wamenipa ulinzi, magari manne kiujumla na nikaambiwa kuwa nisidharau ni jambo la hatari ya hali ya juu.

Kwa sasa nachukuliwa kama adui wa serikali na ni kwa sababu tu naikosoa pale ambapo kunakuwepo na ukiukwaji unaofanyika na serikali hiyo”, amesema Twagiramungu.

“Suala la kupotea kwa watu katika mazingira ya kutatainisha, ni uhalifu, kwani kuna mateso fulani zinayoyapata familia za wahanga na marafiki zao”, amesema, Daniel Bekele, mkuu wa HRW katika kanda ya Afrika.

Daniel Bekele, amesema polisi na maafisa wa sheria nchini Rwanda wanalazimika kwa hali na mali kuanzisha uchunguzi wa kina kuhusu kupotea kwa watu hao katika mazingira ya kutatanisha.

HRW inasema kulingana na taarifa ilizokusanya, baadhi ya watu waliyopotea katika mazingira ya kutatanisha wanasadikiwa kuwa wafuasi au wanaoshirikiana na kundi la waasi kutoka jamii ya Wahutu (FDLR).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.