Pata taarifa kuu
JAMHURI YA KIDEMOKRAISIA YA CONGO-Usalama

Wanajeshi 6 wa FARDC wauawa mashariki mwa DRC

Wanajeshi sita wa jeshi la serikali, FARDC waliuawa katika shambulizi liliyotekelezwa na wapiganaji wa mai mai wa Kundi la APCLS dhidi ya ngome ya jeshi hilo katika mji wa Nyabondo,mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, taarifa kutoka Umoja wa Mataifa, MONUSCO zimethibitisha.

Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo FARDC wakiwa katika operesheni  kaskazini mwa mji wa Goma.
Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo FARDC wakiwa katika operesheni kaskazini mwa mji wa Goma. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yamefanywa na kundi linalofahamika kama muungano wa ukombozi wa Kongo huru, APCLS, katika eneo la Nyabyondo umbali wa kilomita 70 kaskazini mwa Goma katika mtaa wa Masisi, jimboni Kivu Kaskazini.

Msemaji wa jeshi la Umoja wa mataifa MONUSCO, Felix Prosper Baase, amewaambia waandishi wa habari katika mkutano wa Jumatano jana mjini Kinshasa kwamba mmoja wa wanajeshi wake pamoja na wanajeshi wengine walijeruhiwa katika tukio hilo.

Aidha ameeleza wanajeshi hao na wale wa serikali wamefanikiwa kudhibiti upya ngome yao hiyo huko Kivu Kaskazini.

Waziri wa habari akiwa pi msemaji wa serikali ya DRC, Lambert Mende.
Waziri wa habari akiwa pi msemaji wa serikali ya DRC, Lambert Mende. ©RFI/Delphine Michaud

Wakati huo huo serikali ya Kinshasa imetangaza orodha nyingine ya watu mia moja ambao wamepewa msamaha na rais Joseph Kabila akiwemo mbunge Muhindo Nzangi Bitondo aliyehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kumtusi Rais mwaka uliopita.

Hata hivyo, serikali ya DRC inawataka wananchi kutohatarisha usalama wa watu hao waliosamehewa au kuwanyanayapaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.