Pata taarifa kuu
MISRI-Sheria

Misri: wafuasi 700 wa Morsi wahukumiwa kwa pamoja adhabu ya kifo

Kiongozi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood Mohamed Badei, pamoja na watu 700 wanao shukiwa kuwa wafuasi wa rais aliepinduliwa madarakani Mohamed Morsi nchini Misri wamehukumiwa mapema leo asubuhi na Mahakama moja katika mji wa Minya adhabu ya kifo.

Kiongozi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood Mohamed Badei.
Kiongozi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood Mohamed Badei. REUTERS/Mohamed Abd El-Ghany/
Matangazo ya kibiashara

Mahakama hio , katika mji wa Minya, katikiati mwa nchi, imewapunguzia adhabu ya kifungo cha maisha jela iliyotolewa yapata sasa mwezi moja dhidi ya zaidi ya wafuasi 500 wa vuguvugu la Muslim Brotherhood.

Baadhi ya wafuasi wa vuguvugu la Muslim brotherhood ambao wanakabiliwa na adhabu ya kifo.
Baadhi ya wafuasi wa vuguvugu la Muslim brotherhood ambao wanakabiliwa na adhabu ya kifo. REUTERS/Al Youm Al Saabi Newspaper

Watu hao walihukumiwa kwa pamoja, jambo ambalo halijawahi kufanyika katika historia ya nchi hio, wakituhumiwa kushiriki katika maandamano yaliyosababisha machafuko katika mji wa Minya agosti 14, ambapo wafuasi 700 wa Mohamed Morsi waliuawa kwa risase ziliyopigwa na askari polisi na wanajeshi katika mji wa Cairo.

Mashirika ya Kimataifa ya kutetea haki za binadamu na Mataifa ya Magharibi yamekosoa uamuzi wa Mahakama hiyo ya Misri na wanaitaka kubadilisha uamuzi huo.

Mamia ya wafuasi wa Muslim brotherhood kundi ambalo limepingwa marufuku nchini humo waliuawa na wengine kuzuiliwa kutokana na machafuko ya kisiasa yaliyotokea nchini humo.
Machafuko ya kisiasa yalianza kushuhudiwa nchini Misri baada ya kuondolewa madarakani kijeshi kwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemomkrasia Mohammed Mosri.

Watu hao walihukumiwa kifo kwa mara ya kwanza mwezi machi baada ya kesi kufanyika kwa takriban saa moja, kesi ambayo ilizua shutuma kali kutoka jumuiya ya kimataifa.

Mawakili wa utetezi walinyimwa fursa ya kujieleza na hata mashtaka hayakutangazwa.
Baadaye kesi hiyo iliwasilishwa mbele ya mmoja wa viongozi wakuu wa kidini ili kuamuliwa tena lakini maoni yake hayakuzingatiwa.

Miongoni mwa waliohukumiwa kunyongwa ni vijana wawili wenye umri wa miaka 17, mtu mmoja mlemavu na wakili aliyewakilisha baadhi ya washukiwa hadi alipokamatwa.
Kabla ya uamzi huo wa mahakama kutangazwa mawakili wa washtakiwa walisema watakata rufaa iwapo mahakama itapitisha hukumu zilizotolewa.
Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.