Pata taarifa kuu
DRC-Usalama

Kiongozi wa waasi wa Maimai Simba auawa DRC

Paul Sadala maarufu kwa jina la " Morgan", ambaye alikua kiongozi wa waasi wa Maimai Simba wenye asili ya Ituri kaskazini-mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ameuwawa jana na askari wa FARDC nchini humo, baada ya kujisalimisha mwishoni mwa juma lililopita.

Hifadhi ya kitaifa ya  wanyama ya Virunga, mashariki mwa DRC, kunakodaiwa kujificha makundi ya waasi.
Hifadhi ya kitaifa ya wanyama ya Virunga, mashariki mwa DRC, kunakodaiwa kujificha makundi ya waasi. AFP/ALAIN WANDIMOYI
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo vinavyoaminika, muasi huyo ameuawa wakati akihamishwa kutoka kijijini kwake Badengaido kwenye umbali wa kilomita 300 kusini-magharibi mwa Bunia kuelekea mji huo katika mazingira ya kutatanisha.

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Congo, Morgan ameuawa wakati yeye na washirika wake wengine 42 walkua wakijaribu kukimbia huku wakiwafyatulia risasi askari wa FARDC waliokuwa wanawasindikiza katika uhamisho huo.

Waziri wa mawasiliano akiwa pia msemaji wa serikali ya DRC, Lambert Mende, amesema Morgan amefariki akiwa ndani ya helikopta ya kikosi cha Umoja wa mataifa nchini jamhuri ya Kidermokrasia ya Congo.

“Ghafla Morgan aliamua kutaka kuwakwepa askari wa FARDC baada ya kujipatia silaha kadhaa na kuanzisha mashambulizi dhidi ya askari wa FARDC ambao wawili wamefariki na wawili miongoni mwa wapiganaji wake pia wamefariki, yeye mwenyewe amejeruhiwa vibaya mguuni na ndivyo alivyotakiwa kuelekea Mambasa na Komanda kwa kutumia Helikopta ya Monusco hadi Bunia, basi alipokuwa akipelekwa kwenye helikopta ndipo alipofariki”, amesema Mende.

Madai hayo ya serikali ya Kinshasa yanatupiliwa mbali na vikosi vya kulinda amani vya Monusco ambavyo vinahakikisha kwamba Morgan alikuwa ameuwawa tayari hata kabla ya kuuleta mwili wake kwenye helikopta ya Monusco ambapo imeanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha kifo chake.

Hayo yakijiri marubani watano wa jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo DRC wamejeruhiwa kwenye shambulio la bomu la kutegwa barabarani, shambulio lililotekelezwa kwenye barabara ya beni mjini Mavivi ambapo marubani hao walikuwa wakielekea uwanja wa ndege.

Shambulio hili la bomu la kutegwa linaelezwa kutaka kuulenga msafara wa viongozi wa juu wa jeshi la FARDC ambao walipita kwenye barabara hiyo saa chache kabla ya kutokea mlipuko ambao uliwajeruhi marubani waliokuwa kwenye basi dogo.

Tukio hilo limetokea umbali wa kilometa tano kusini mwa mji wa Mavivi ambapo wanajeshi hao walipelekwa kwenye hospitali jirani kwa matibabu huku uchunguzi wa awali ukilinyooshea kidole kundi la ADF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.