Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Wananchi wa Rwanda waadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994

media Kanisa la Ntarama, ambako wakimbizi elfu tano kutoka jamii ya watutsi waliyouawa aprili 15 mwaka 1994. RFI/N.Champeaux

Wananchi wa Rwanda wameadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 tangu kutokea kwa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yaliosababisha vifo vya watu laki nane kwa kipindi cha siku mia moja. Maadhimisho hayo yamefanyika jijini Kigali na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Barani Afrika na wawakilishi wa mataifa ya magharibi pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ambaye amesema Jumuiya ya kimataifa bdo inajuta kwa kutozuia mauaji hayo.

Katika hotuba yake rais Paul Kagame amesisitiza kuwa Historia ya mauaji hayo ya kimabari hayawezi kufutika na kuyataka baadhi ya mataifa kama Ufaransa kukiri wazi kuwa ilishiriki katika mauaji hayo.

Katika hatuwa nyingine, ujumbe wa Ufaransa uliotarajiwa kuwasili nchini Rwanda kushiriki kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka ishirini tangu mauaji ya kimbari yatokee nchini humo umeamua kutoshiriki.

Hata balozi wa Ufaransa mjini Kigali, ambae ametakiwa kuliwakilisha taifa lake, amefahamisha kwamba hatoshiriki katika sherehe hizo, akibaini kwamba hakupata kibali maalumu kinachotolewa na itifaki ya Rwanda kwa viongozi wanaohudhuria sherehe ya maadhimisho ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari.

Christiane Taubira, waziri wa sheria wa Ufaransa. Reuters/Charles Platiau

Waziri wa sheria wa Ufaransa Christiane Taubira alitarajiwa kuongoza ujumbe huo, lakini hatua ya kusitisha ushiriki wa nchi hiyo unatokana na matamshi ya viongozi wa Rwanda kuendelea kuituhumu Ufaransa kuhusika kwa njia moja au nyingine kwa kile kilichotokea nchini Rwanda mwaka 1994, wakati Ufaransa ilikua iliwatuma wanajeshi wake kuwalindia usalama raia katika maeneo yaliyokua yalitengwa, ambayo yalijulikana kwa jina la “zone turquoise”.

Kauli hiyo ya rais Kagame haikutofautiana na ya waziri wake wa mambo ya ndani Louise Mushikiwabo ambaye amekosoa hatua ya serikali ya Ufanaransa kusitisha ushiriki wao kwenye sherehe hizo na kusema kuwa licha ya hayo, bado historia ina nafasi yake.

Katika hatua nyingine, rais Kagame amegusia mahusiano ya nchi yake na baadhi ya nchi nyingine ikiwemo Afrika Kusini ambayo imeghadhabishwa na ushiriki wa baadhi ya wanadiplomasia wa Rwanda katika jaribio la kumuua Jenerali Faustin Kayumba Nyamwasa, na kubainisha kuwa bado nchi yake inahitaji uhusiano mzuri na Afrika kusini kwa vile bado tuhuma hizo hajizathibitishwa.

Rais Kagame ataongoza sherehe hizo kwenye uwanja wa mpira wa Amahoro, ambapo wakiwepo baadhi ya marais na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, huku nchi ya Burundi nayo ikiazimisha kumbukumbu ya miaka ishirini ya rais wao Cyprien Ntaryamira ambaye aliuawa kwenye ndege pamoja na rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyarimana.

Watu 800.000 kutoka jamii ya watutsi na wahutu waliyokua wakipinga utawala wa rais Juvenal Habyarimana, waliuawa baada ya ya rais huyo kufariki katika ajali ya ndege iliyodunguliwa kwenye uwanja wa ndege wa Kanombe mjini Kigali, tarehe 6 kuamkia 7 aprili mwaka 1994.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana