Pata taarifa kuu
Zimbabwe-siasa

Viongozi wa chama cha upinzani nchini Zimbabwe cha MDC watofautiana kuhusu suala la kuandaa mkutano wa makati kuu ya chama

Katibu mkuu wa chama cha upinzani nchini Zimbabwe MDC, Tendai Biti ameendelea kuvutana na mwenyekiti wake, Morgan Tsvangirai, safari hii akitaka kiongozi huyo kutoruhusiwa kuwemo wakati wa kikao cha kamati kuu ya chama kujadili suala la Elton Mangoma.

Katibu mkuu wa chama cha MDC Tendai Biti na mwenyekiti wake Morgan Tsvangirai
Katibu mkuu wa chama cha MDC Tendai Biti na mwenyekiti wake Morgan Tsvangirai
Matangazo ya kibiashara

Mvutano huo ulianza kushuhudiwa toka juma lililopita punde tu baada ya tangazo la kamati ya utendaji kutangaza kumsimamisha kwa muda naibu mweka hazina Elton mangoma kufuatia matamshi yake ya kumtaka kiongozi wa chama hicho kuachia ngazi.

Lakini katika kile kinachoonekana kuwa bado kuna mgawanyiko ndani ya chama hicho hata katibu mkuu wake Tendai Biti anaonekana kutofautiana na mwenyekiti wake kuhusu kuruhusiwa kushiriki wakati wa mkutano wa kamati kuu ya chama.

Wachambuzi wa mambo wameonya kuhusu kuendelea kushuhudiwa kwa tofauti ndani ya chama hicho na kwamba kunatoa mwanya kwa chama tawala cha ZANU-PF kuendelea kujipatia umaarufu.

Hofu ya kushuhudiwa mgawanyiko zaidi ndani ya chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for democratic Change MDC, imeendelea kutanda wakati huu ambapo uongozi wa chama hicho ukiwataka viongozi waliochoka kuwemo ndani ya chama hicho kujiondoa wenyewe.

Msimamo wa chama hicho umetolewa mwishoni mwa juma na rais wake, Morgan Tsvangirai ambaye ameendelea kusisitiza kuwa hatoondoka madarakni kwa shinikizo la viongozi wachache wenye kutaka kumpindua.

Kauli ya Tsvangirai ameitoa ikiwa zimepita siku mbili tu, toka chama hicho kitangaze kumsimamisha kwa muda naibu mweka hazina wa chama hicho, Elton Mangoma kufuatia matamshi yake ya hivi karibu kumtaka kiongozi huyo kujiuzulu.

Mangoma sasa anasubiri uamuzi wa kamati ya nidhamu ya chama hicho ambayo itaketi hivi karibuni kuamua hatma yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.