Pata taarifa kuu
Cote d Ivoire

Waliosababisha ajali na vifo vya watu 63 wakati wa Sherehe za mwaka mpya nchini Cote d Ivoire kuchukuliwa hatua

Uchunguzi juu ya sababu ya kutokea vifo vya watu 63 wakati wa shamrashamra za mwaka mpya jijini Abidjan nchini Cote d Ivoire umetoa ripoti yake ikitoa lawama juu ya uwepo wa askari wachache wa kusimamia hali ya usalama katika eneo la tukio.

Baadhi ya watu walionusurika katika ajali wakati wa sherehe za mwaka mpya jijini Abidjan
Baadhi ya watu walionusurika katika ajali wakati wa sherehe za mwaka mpya jijini Abidjan REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Sababu kubwa iliyoelezwa ni kutokuwepo kwa vikosi vya usalama vya kutosha na uwepo wa uzio ambao ujenzi wake ulikuwa ukiendelea hali iliyosababisha eneo hilo kuwa jembamba na kusababisha hali ya msongamano mkubwa wa watu walipokuwa wakitoka katika viwanja hivyo, Mwendesha mashtaka wa mjini Abidjan Simplice Kouadio Koffi ameeleza.
 

Koffi amesema kuwa kutokana na Ripoti hiyo atachukua hatua za kisheria dhidi ya wale wanaoelezwa kuwa walikuwa na jukumu la kuhakikisha usalama unakuwepo viwanjani hapo.
 

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka huyo, Wafanyakazi kadhaa wa Serikali na Idara ya Uokozi wanahojiwa juu ya Ajali hiyo, baada ya maombolezo ya siku tatu kitaifa yaliyotangazwa na Rais Alasane Ouattara.
 

Chama cha upinzani cha Rais wa Zamani nchini Cote d Ivoire, Laurent Gbagbo kimemtaka Waziri wa mambo ya ndani wa Nchi hiyo Hamed Bakayoko, kujiuzulu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.