Pata taarifa kuu
DR Congo

Kesi ya Rufaa juu ya kuuawa kwa Mwanaharakati Floribert Chebeya kusikilizwa leo jijini Kinshasa

Kesi ya rufaa ya askari Polisi wanaotuhumiwa kwa mauaji Floribert Chebeya wa Shirika la kutetea haki za Binadam La Voix des sans voix, inatarajiwa kusikilizwa tena leo hii jijini Kinshasa.

Generali John Numbi anayetakiwa kujibu tuhuma za kuhusika na Mauaji ya Floribert Chebeya
Generali John Numbi anayetakiwa kujibu tuhuma za kuhusika na Mauaji ya Floribert Chebeya © Passerelle
Matangazo ya kibiashara

Baada ya ushahidi uliotolewa na mtuhumiwa Paul Mwilambwe anayedai kushuhudia mauwaji hayo, Mashirika ya kiraia yanaendelea kuamini kuwa Mahakama itaitikia ombi lao la kumtaka Jenerali Numbi kujibu tuhuma za mauwaji ya Chebeya.

Wiki moja iliyopita Meja Paul Mwilambwe, ambaye ni askari polisi aliyekimbilia nje kuhofia usalama wake aliwatuhumu si tu Jenerali Numbi, lakini pia Rais Joseph Kabila kuamuru mauaji hayo.

Katika hatua nyingine Waasi wa M23, wanaodhibiti eneo la Mashariki mwa Congo wametishia kuendelea na harakati zao hata kudhibiti sehemu kubwa zaidi ya Nchi hiyo ikiwa Serikali ya Joseph Kabila atakataa kufanya Mazungumzo ya Amani.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amekuwa akisimamia mazungumzo ya amani kati ya Serikali ya Kinshasa na M23, lakini waasi hao wamekuwa wakitaka mazungumzo ya makubaliano ya Moja kwa moja na Rais Kabila.

Siku ya Jumamosi kundi hilo lilibadili jina na kujiita Congolese Revolutionary Army na kusema kuwa linajiandaa kukabiliana na Mashambulizi mapya yatakayotekelezwa na Jeshi la Congo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.