Pata taarifa kuu
SUDAN-SUDAN KUSINI-ETHIOPIA

Jeshi la Sudan limefanikiwa kuwasambaratisha Waasi wa SPLM-North katika Jimbo la Blue Nile

Jeshi la Polisi nchini Sudan limekabiliana vikali na waasi na kufanikiwa kukomboa maeneo ambayo yalikuwa yanashikiliwa karibu kabisa na mpaka wake na jirani zao wa Sudan Kusini taarifa kutoka Khartoum zimethibitisha.

Waasi wa SPLM-North ambao wamerudishwa nyuma na wanajeshi wa serikali ya Sudan katika Jimbo la Blue Nile
Waasi wa SPLM-North ambao wamerudishwa nyuma na wanajeshi wa serikali ya Sudan katika Jimbo la Blue Nile
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Sudan linachukua utawala wa maeneo hayo kipindi hiki ambacho juhudi za kumaliza machafuko baina yake na jirani zao wa Sudan Kusini zikiendelea na viongozi wa mataifa hayo wanatarajiwa kukutana mwishoni mwa juma hili.

Sudan imekuwa ikiilaumu Sudan Kusini kufadhili waasi ambao wanapambana nao wa SPLM-North ambao wenyewe wamekana uwepo wa mapigano baina yao na jeshi la serikali Kusini mwa Blue Nile.

Msemaji wa SPLM-North Arnu Lodi ameshindwa kuzungumza chochote juu ya taarifa za wao kusambaratishwa na jeshi la Sudan baada ya kuzuka mapigano makali katika eneo la Sarkam.

Jeshi la Sudan kupitia msemaji wake Al Sawarmi Khalid amejigamba kurejesha eneo la Magharibi mwa Jimbo la Blue Nile kwenye himaya yao na kudhibiti mauaji ya watoto na wanawake ambayo yalikuwa yanafanywa na SPLM-North.

Sudan kupitia jeshi lake limeendelea kupambana na waasi wa SPLM-North ambao wamekita himaya yao kwenye majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile na kutajwa kupata ufadhili kutoka Sudan Kusini.

Sudan na Sudan Kusini licha ya kutuhumiana huko lakini zimeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha zinamaliza mgogoro wake wa kugombea mipaka na maeneo yenye utajiri wa mafuta.

Umoja wa Afrika AU umekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha unapata suluhu ya mgogoro wa mipaka na umiliki wa maeneo yenye utajiri hasa kwenye majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.