Pata taarifa kuu
Cote d'Ivoire

Benki ya Dunia kusaidia Cote d Ivoire kujiimarisha kiuchumi

Rais Mpya wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim, ameanza ziara yake barani Afrika kwa kutoa wito kwa Serikali ya Cote d Ivoire kutafuta amani ili kukuza uchumi wa nchi hiyo.

Rais wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim
Rais wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim
Matangazo ya kibiashara

Kim mwenye umri wa Miaka 52 aliyeanza kutumikia wadhifa wake mwezi July, alikutana na Rais wa nchi hiyo, Alassane Ouattara kwa ajili ya Mazungumzo.
 

Kim ameiambia Cote d Ivoire kuwa ili nchi hiyo kukua kiuchumi ni budi kuwashirikisha Wanawake, halikadhalika kuwapatia ajira vijana.
 

Ouattara ambaye aliwahi kuwa katibu Mtendaji wa Shirika la fedha duniani, IMF alieleza matumaini yake kuwa Benki ya Dunia itaisaidia nchi yake zaidi kwa kuipa Misaada ya kiuchumi, ambayo amesema ilimsaidia kufanya mabadiliko mbalimbali kutoka kwenye mdororo wa kiuchumi mpaka kukua kwa uchumi kwa Asilimia nane mwaka huu.

Katika mazungumzo yake na Ouattara, ambaye kwa sasa anaiongoza jumuia ya kiuchumi ya nchi za Magharibi mwa Afrika,ECOWAS, Kim alitathmini Matatizo ya ukanda huo na namna ambavyo Benki ya Dunia itasaidia katika kupata Suluhu.

Benki ya Dunia imetenga kiasi cha Dola bilioni moja kwa ajili ya Mipango ya maendeleo kwa ajili ya Cote d Ivoire.
 

Mkuu huyo amekamilisha ziara yake nchini humo na anatarajiwa kuwasili Afrika kusini ambapo atakutana na Rais Jacob Zuma.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.