Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Julius Malema kufikisha mashtaka mahakamani

Katika kile kinachoonekana ni kutokata tamaa licha ya kufukuzwa uanachama wa chama tawala nchini Afrika kusini, aliyekuwa rais wa Umoja wa Vijana wa Chama cha ANC Julius Malema amesema kuwa atahakikisha shauri lake la kupinga kufutwa uanachama linafika mahakamani.

Kiongozi wa Umoja wa Vijana wa ANC Julius Malema ambaye amefutwa uanachama na kamati ya nidhamu
Kiongozi wa Umoja wa Vijana wa ANC Julius Malema ambaye amefutwa uanachama na kamati ya nidhamu Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mwezi wa pili mwaka huu kamati ya nidhamu ya chama hicho iliketi na kuazimia kumfuta uanachama Julius Malema baada ya kumkuta na hatia ya kushiriki njama za kukigawa chama kwa kupandikiza chuki na kuhamasisha mapinduzi kwenye nchi nyingine.

Akizungumza kwenye mji alikozaliwa wa Limpopo, Malema amesema kuwa hata kaa kimya kamwe na kuona haki yake ikipotea badala yake amepanga kufikisha shauri lake katika mahakama kuu.

Awali kiongozi huyo zamani wa tawi la vijana katika chama ANC Julius Malema alikataa hawezi kwenda mahakamani, lakini kwa sasa amebadili msimamo huo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.