Pata taarifa kuu
Uganda

Kiongozi wa Upinzani nchini Uganda Kizza Besigye akamatwa

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa na polisi  baada ya kuongoza maandamano jijini Kampala siku ya Jumatano kulalamikia kupanda kwa bei za bidhaa, maandamano ambayo polisi inasema  hayakuwa  halali.

Polisi jijini Kampala Uganda wakimkamata kiongozi wa Upinzani Kizza Besigye
Polisi jijini Kampala Uganda wakimkamata kiongozi wa Upinzani Kizza Besigye
Matangazo ya kibiashara

Wakili wake,Ernest Kalibala hata hivyo anasema Besigye atafunguliwa mashtaka ya kuongoza maandamano yasiyo halali na ataachilia huru kwa dhamana.

Besigye alikamatwa pamoja na wanaharati wengine 16 huku polisi wakiwapiga wafuasi wa upinzani na kuwarushia gesi za kutoa machozi na kusambatarisha maandamano hayo.

Polisi mmoja aliuawa katika purukushani hizo ambazo polisi wanasema mwenzao alipigwa jiwe kichwani akiwa katika harakati za kuwasambaratisha wafuasi hao.

Inaelezwa pia kuwa waandishi wa habari wawili walipigwa na polisi katika vurugu hizo siku ya Jumatano, suala ambalo muungano wa kutetea haki za waandishi habari umekashifu vikali.

Besigye ambaye atafikishwa Mahakamani Ijumaa,amekuwa akikamatwa na polisi na kuachiliwa huru kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita kutokana na tuhma za kuongoza maandamano ya umma kulalamikia kupanda kwa bei ya bidhaa nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.