Pata taarifa kuu
MISRI

Mke wa Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak awekwa kizuizini

Mke wa Rais aliyeondolewa madarakani na nguvu ya umma nchini Misri Hosni Mubarak, Suzanne Thabet ataendelea kuwa kizuizini wakati uchunguzi dhidi ya mali anazomiliki ukiendelea kushika kasi.

Vurugu zilizotokea nchini Misri kati ya waumini wa Dini ya Kiislam na Kikristo
Vurugu zilizotokea nchini Misri kati ya waumini wa Dini ya Kiislam na Kikristo REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na Mali Haramu Assem Al Gohari ametoa siku kumi na tano kwa Suzanne kuendelea kushikiliwa kizuizini wakati uchunguzi wa utajiri wake ukiendelea.

Shirika la Habari la MENA limeonesha tamko hilo kutoka kwa Al Gohari wakati huu ambapo duru za Kiusalama kizieleza Suzzane huenda akapelekwa katika Gereza la Qanater ambalo lipo nje ya Jiji la Cairo.

Mamlaka hiyo imetoa siku 15 pia kwa Hosni Mubarak baada ya kuhojiwa kwa saa tatu pamoja na Mkewe Suzanne ambao wanakabiliwa na tuhuma za kujilimbikizia mali.

Hii ni mara ya kwanza kwa Mubarak kuhojiwa na Kitengo hicho kilicho chini ya Wizara ya Sheria kikiwa na wajibu wa kuangalia uhalali wa mali za familia hiyo ya Rais wa zamani.

Mubarak alianza kushikiliwa tarehe 13 ya mwezi April ambapo kwa sasa yupo katika Hospital ya Sharm El Sheikh akipatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo.

Watoto wawili wa Mubarak ambao ni Alaa na Gamal nao wote wanakabiliwa na kesi za kujibu huku wakizuia kusafiri nje ya Misri huku mali ambazo zilikuwa zinamilikiwa na familia hizo zikishikiliwa na serikali.

Katika hatua nyingine maelfu ya Waumini wa Kiislam na Kikristo wamefanya maandamano katika Mji Mkuu Cairo lengo likiwa ni kuhimiza mshikamano baada ya kushuhudia mapigano ya kidini yaliyozuka juma lililopita.

Mashambulizi hayo ya kidini yalisababishwa watu kumi kupoteza maisha huku wengine mamia wakijeruhiwa baada ya waumini wa Kiislam na Kikristo kushambuliana.

Waandamanaji waliojitokeza katika Viunga vya Tahrir wameimba nyimbo za kuhamasisha uwepo wa amani katika taifa hilo sambamba na kuunga mkono juhudi za kuungana kwa vyama hasimu nchini Palestina vya Hams na Fatah.

Tangu kufanyika kwa mapinduzi nchini Misri na kushuhudia Hosni Mubaraka akiondolewa madarakani wananchi wa taifa hilo wamekuwa na utaratibu wa kukutana kwenye viunga vya Tahrir kila kunapokuwa na kitu kipya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.